Na khalil ibrahim
KILA binadamu hapa duniani ana haki ya kuishi. Kutokana na hali hiyo kumekuwa na wadau pamoja na Taasisi mbalimbali zinazopigania kuona haki hizo zinalindwa.
Hivyo basi, katika matumizi ya usafiri wa vyombo vya nchi kavu na majini,Baraza la Ushauri watumiaji wa vyombo hivyo (SUMATRA-CCC)limekuwa mstari wa mbele kupigania haki hizo.
Baraza la Sumatra-ccc linaamini kuwa binadamu anayo haki ya msingi kama zilivyoelezwa na shirika la kimataifa la muungano wa watumiaji wa huduma hiyo (International Organization of Consumers Union (IOCU).
Baraza la Sumatra-ccc liliundwa kwa mujibu wa kifungu cha 29, sheria namba 9, ya mamlaka ya usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA) ya mwaka 2001.
Baraza hilo lilianzishwa Agosti 2004 na kuzinduliwa rasmi Oktoba 17 mwaka 2005 na majukumu yake ni kushughulikia masilahi ya watumiaji wa huduma kwa kuwasilisha maoni na taarifa mbalimbali kwa SUMATRA na waziri mwenye dhamana pamoja na sekta husika.
Kupokea na kusambaza taarifa na maoni kuhusu masuala yanayowagusa watumiaji wa huduma zinazosimamiwa na SUMATRA.
Pia baraza hilo linashauriana na wadau, serikali na makundi ya watumiaji kuhusu huduma na kuunda kamati za watumiaji wa huduma za usafiri wa majini na nchi kavu katika mikoa na kushauriana nazo.
Haki ambazo zimeanishwa na shirika la kimataifa (IOCU) zipo kumi na mbili ambazo ni haki ya kupata mahitaji mhimu, usafiri endelevu na wenye kuzingatia nidhamu, maslahi ya kila mmoja ni moja ya mahitaji muhimu, kwa hiyo kila mtu anayo haki ya kupata usafiri endelevu na wenye kuzingatia heshima na utu wa kila mmoja.
Haki ya Usalama; Abiria anapokuwa safarini ana haki ya kusafirishwa na basi, gari moshi au meli ambayo ni salama na ambayo itamfikisha aendapo salama na chombo ambacho hakikidhi haki hii hakipaswi kusafirisha abiria.
Haki ya kupewa taarifa; abiria ana haki ya kupewa taarifa sahihi kabla ya kuanza safari na awapo safarini juu ya safari yake, ana haki ya kujua safari inaanza saa ngapi na atatumia muda gani safarini n. k.
Haki ya kuchagua; abiria ana haki ya kuchagua ni usafiri gani atumie, kwa hiyo abiria ana haki ya kuchagua kulingana na mahitaji yake ya muda huo.
Haki ya kuchagua; abiria ana haki ya chaguo kulingana na mahitaji yake ya muda huo.
Haki ya kulipwa fidia; abiria akipata hasara ya aina yoyote ambayo imesababishwa na uzembe wa mwenye chombo cha usafiri, kama vile kucheleweshwa, kuumia au kudhalilishwa, abiria ana haki ya kulipwa fidia.
Haki ya kuelekezwa; abiria ana haki ya kuelimishwa juu ya haki zake, Baraza la ushauri la SUMATRA-CCC linatekeleza azma hiyo ya kuwaelimisha watumiaji wa huduma za usafiri wa nchi kavu na majini.
Haki ya kusafiri katika mazingira salama; abiria ana haki ya kutokusumbuliwa au kusumbua abiria wengine awapo safarini.
Vitendo ambavyo vinaleta usumbufu wa aina yoyote kwa abiria wengine ikiwa ni pamoja na kupiga kelele ovyo, kuchafua mazingira ndani ya chombo cha usafiri, ikiwa ni pamoja na kuvuta sigara na vitu vingine vinavyoweza kumpa kero, haviruhusiwi.
Haki ya kupata mahitaji muhimu; mtumiaji wa huduma za usafiri wa nchi kavu na majini anawajibu wa kutumia vyombo hivyo kwa makini.
Haki ya usalama; mtumiaji wa usafiri wa nchi kavu na majini anawajibu wa kuwa makini na chombo anachotarajia kukitumia katika safari zake.
Haki ya kupewa taarifa; Mtumiaji wa usafiri wa nchi kavu na majini ana wajibu wa kutafuta taarifa zilizopo kwa ajili ya kujiridhisha kabla ya kuchagua chombo cha kusafiria.
Haki ya kuchagua; mtumiaji wa huduma ya usafiri wa nchi kavu na majini anawajibu wa kufanya chaguo la chombo cha usafiri baada ya kupata taarifa zinazokidhi mahitaji yake.
Haki ya kulipwa fidia; mtumiaji wa huduma za usafiri majini na nchi kavu ana wajibu wa kupigania usafiri unaokidhi mahitaji yake.
Abiria akipata hasara ya aina yoyote ambayo imesababishwa kwa uzembe wa mwenye chombo cha usafiri kama vile kucheleweshwa, kuumia na kudhalilishwa, abiria ana wajibu wa kudai fidia.
Haki ya kuelezwa haki zake /haki ya kuelimishwa; mtumiaji wa huduma za usafiri wa nchi kavu na majini ana wajibu wa kutafuta taarifa sahihi.
Webste:www.mobinday.blogspot.com niandikie; mobinsons@yahoo.com 0753 399 579.
HII NI AJALI MBAYA ILITOKEA MWAKA HUU 2010 MKOANI SINGINDA NA KUUA WATU KADHAA ,HUU NI MWENDELEZO WA AJALI AMBAZO BARAZA LA SUMATRACCC LINAFANYA JUHUDI KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA USAFIRI ILI KUZIMALIZA .
No comments:
Post a Comment